1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamala ziarani Tanzania kuimarisha mahusiano ya taifa lake

30 Machi 2023

Makamu wa Rais wa Marekani kamala Harris yupo nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku tatu,akitokea nchini Ghana ambako taifa lake limeahidi kutoa mamilioni ya dola ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi.

https://p.dw.com/p/4PTKN
Kamala Harris beim Abflug aus Ghana Richtung Tanzania
Picha: Misper Apawu/AP/picture alliance

Akiwa katika taifa hilo la Afrika mashariki ambapo Marekani imekuwa ni mshirika mkubwa wa maendeleo atafanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan yanayonuia kuimarisha mahusiano baina ya pande mbili.

Duru zinaarifu kuwa miongoni mwa mambo yanayotarajiwa kugusiwa katika mazungumzo baina ya viongozi hao, ni pamoja na maendeleo ya kiuchumi,mabadiliko ya tabia nchi,usalama wa chakula pamoja na maendeleo ya democrasia.

Kando na mazungumzo yatayolenga kuimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili, mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu Marekani atatembelea Makumbusho ya Taifa na kumbukumbu ya ulipuaji wa Ubalozi wa Marekani mjini humo.

Soma pia:Makamu wa rais wa Marekani aanza ziara yake katika nchi tatu barani Afrika ambapo yuko nchini Ghana

 Kamala akiwa katika jiji hilo ambalo ni kitovu cha biashara Tanzania,atakutana pia na wajasiriamali wa tabaka mbalimbali.

Marekani kupitia mashirika yake imekuwa ikiendesha miradi kadhaa nchini humo ya kuhamasisha kuinua pato la wananchi hasa wanawake na vijana kupitia kila sekta.

Maoni ya wachambuzi katika ziara hiyo

Wachambuizi wa masuala ya siasa na diplomasia,wanaitazama ziara hiyo ya Marekani barani Afrika ni kukabiliana na ushawishi ya Urusi na China unaoongezeka.

China imewekeza pakubwa barani Afrika lakini Marekani inajipanga kama mshirika bora kuliko China.

Mwishoni mwa mwaka huu rais Joe Biden pia anatarajiwa kuzuru Afrika,wakati mkewe Jill Biden,waziri wa fedha Janet Yellen na waziri wa mambo ya nje Antony Blinken walikuwa barani humo.