1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Davos mjadala watawala ushirika wa China kimataifa

18 Januari 2023

China kutangaza kufungua milango yake kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa kunatajwa na wachumi kunaweza kubadili uchumi wa dunia kutokana na utayari wake wa mashirikiano, hayo yamejiri kwenye jukwaa la uchumi Davos

https://p.dw.com/p/4MMHl
Weltwirtschaftsforum in Davos, Liu He
Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Naibu waziri mkuu wa China Liu alitzoa hotuba yake kwenye jukwaa hilo la uchumi duniani kwa mwaka 2023 mjini Davos hapo jana.

Akisisitiza taifa lake ambalo linauchumi mkubwa duniani daima linatazama maendeleo ya kiuchumi kama jukumu lake muhimu, na kusisitiza ahadi ya China kufunguamilango linapokuja suala la ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kukuza  uchumi wake dunia na utandawazi kwa ujumla wake.

Mataalamu wa masuala ya uchumi na Mkurugenzi Mtendaji, katika Jukwaa la Uchumi Duniani Jeremy Jurgens amesema ni mapema mno kusema iwapo dunia inaelekea kwenye mdororo wa kiuchuni.

Soma pia:Mkutano wa uchumi wa dunia waanza mjini Davos

Ameongeza kujitolea kwa China katika ushirikiano wa kimataifa kutakuwa na mabadiliko makubwa katika uchumi wa dundia.

Akichangia katika mjadala amesema haujaonekana ushirikiano thabiti hasa masuala mengi muhimu ya kimataifa ambayo yanaweza kutatuliwa kwa ushirikiano.

"Hakika kuna viwango vya juu vya mgawanyiko kisiasa na hata kiuchumi duniani." Alisema na kuongeza kuwa kwa sasa dunia inahitaji ushirikiano thabiti.

Mtazamo wa wachumi katika ushirika wa China

Uchumi wa dunia ambao unaonekana kukumbwa na changangamoto kadha wa kadha ikiwemo majanga ya kiuchumi na kibinadamu unazidi kuwaleta pamoja wachumi ili kuleta ahueni.

Nchi tajiri kiuchumi zatakiwa kupunguza umasikini duniani

Waziri Mkuu wa zamani wa Australia Kevin Michael Rudd,amesema ukuaji thabiti wa uchumi wa China ukilinganisha na uchumi wa dunia utachangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi wa dunia kwa miaka ijayo.

Soma pia:China yasisitiza juu ya kuendeleza uwekezaji wa kigeni

Kwa uande mwingine Saudi Arabia kupitia waziri wake wa masuala ya fedha Mohammed al-Jadaan mesema China ni mshirika muhimu kwa taifa lake katika masuala ya biashara, lakini Marekani ni muhimu zaidi na mshirika wa kimkakati katika masuala ya kiuchumi.

"Tulipitia migogoro kadhaa ya kutokubaliana, lakini haiondoi kuwa sisi ni washirika wa kimkakati na muhimu kwa dunia" Alisema waziri wa fedha Mohammed.

Hotuba muhimu zinazosubiriwa

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky,wanatarahji kuhutubia kongamano hilo la uchumi la mwaka huu la Davos.

Schweiz Davos | Weltwirtschaftsforum | Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa kwenye jukwaa la uchumi Davos Uswis 2022Picha: Arnd Wiegmann/REUTERS

Hizi ni miongoni mwa hotuba muhimu katika jukwaa hilo kwa mwaka huu wa 2023 huku Ujerumani ikikabiliwa na shinikizo la kuipatia Ukraine vifaru vya kivita.

Soma pia:Vita vya Ukraine, mdororo wa uchumi kugubika kongamano la Davos

Ukraine imekuiwa ikipambana na vikosi vya Urusi katika maeneo ya kimkakati wakati vita hivyo vikielekea mwaka pili tangu ilipovamiwa na Urusi.

Scholz ni kiongozi pekee kutoka mataifa yalioendelea kiviwanda ya kundi la G7 kuhutubia kongamano hilo la  kiuchumi kwa mwaka huu anawasili mjini Davos akiwa nawaziri mpya wa masuala ya ulinzi akijiandaa kuanza kazi kazi.