1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Erdogan apanga kujadiliana na Guterres mkataba wa nafaka

5 Septemba 2023

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema nchi yake inafanya mawasiliano ya karibu na Umoja wa Mataifa kuufufua mkataba wa usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia Bahari Nyeusi

https://p.dw.com/p/4VzHh
NATO-Gipfel in Vilnius Erdogan
Picha: LUDOVIC MARIN/AFP

 

Hayo yameripotiwa na vyombo vya habari vya Uturuki siku moja baada ya Erdogan kufanya mazungumzo na rais Vladimir Putin kuhusu mkataba huo ambao Moscow ilijitoa mnamo mwezi Julai. 

Meeting between Putin and Erdogan begins in Sochi

Erdogan amenukuliwa akisema tayari Umoja wa Mataifa unashughulikia matakwa ya Urusi ya kuiwezesha kurejea kwenye mkataba huo ikiwemo kuruhusiwa kwa benki yake ya kilimo kutumia mfumo wa kimataifa wa miamala ya kibenki unaofahamika kama SWIFT.

Kiongozi huyo amesema anapanga kufanya mazungumzo na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres baadaye mwezi huu ili kupigia debe hatua za haraka za kuyashughulikia matakwa muhimu ya Urusi.