1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiZimbabwe

Zimbabwe yawaachia wafungwa kupunguza msongamano magerezani

20 Mei 2023

Zimbabwe imeanza mchakato wa kuwaachilia huru zaidi ya wafungwa 4,000 waliopewa msamaha wa Rais hatua ambayo mamlaka nchini humo zinasema, itasaidia kupunguza msongamano kwenye magereza.

https://p.dw.com/p/4RbVd
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe Picha: Tsvangirayi Mukwazhi/dpa/AP/picture alliance

Karibu wafungwa 800 waliachiliwa huru Ijumaa, kutoka katika gereza kuu na lile la Chikurubi kwenye mji mkuu, Harare.

Kwa mujibu wa msemaji wa huduma za magereza na urekebishaji tabia nchini Zimbabwe, Meya Khanyezi, magereza katika sehemu mbalimbali nchini humo yalianza kuwaachilia wafungwa waliofuzu kupata msamaha wa Rais tangu Alhamisi.

Jela za taifa hilo  zina uwezo wa kuhifadhi wafungwa 17,000 lakini kwa sasa, zina zaidi ya wafungwa 20,000.