1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Yellen asema Marekani haitakubali viwanda vipya kuharibiwa

8 Aprili 2024

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen ameonya kuwa Marekani haitakubali viwanda vipya kuharibiwa na bidhaa za ruzuku kutoka China, kama ilivyokuwa katika sekta ya chuma cha pua nchini Marekani muongo mmoja uliopita.

https://p.dw.com/p/4eYPE
China, Beijing | US-Finanzministerin Janet Yellen
Picha: Tatan Syuflana/AP/picture alliance

Yellen ameuambia mkutano na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara ya siku nne ambapo alikutana na maafisa wa China kwamba mazungumzo baina yao yameimarisha maslahi ya Marekani.

Amesema, wakati soko la kimataifa likifurika bidhaa za bei nafuu za China, masoko ya Marekani na mataifa mengine ya kigeni yanaendelea kubaki mashakani.

Amesema alizungumzia wasiwasi juu ya kupungua kwa mahitaji ya ndani ya China na uwekezaji uliopindukia kwenye viwanda kama vya magari ya umeme, betri na bidhaa za umeme wa jua, uliochochewa na ruzuku kubwa kutoka serikalini.