1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yellen asema mahusiano ya Marekani na China yanaimarika

Amina Mjahid
7 Aprili 2024

Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen amekutana na Waziri Mkuu wa China Li Qiang na kutuma ujume wa ushirikiano wa pamoja licha ya tofauti zao.

https://p.dw.com/p/4eVuW
China
Watiri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen Picha: Pedro Pardo/AFP/Getty Images

Yellen amemwambia Qiang kwamba wana mengi ya kufanya na anaamini kuwa kwa mwaka mmoja uliopita nchi zote mbili zimejaribu kuimarisha mahusiano yao. 

Lakini vile vile akataadharisha kwamba hiyo haimaanishi wanapuuzia tofauti zao ziliopo na kuepuka kuwa na mazungumzo magumu lakini ni vizuri kuelewa kuwa wanaweza kusonga mbele iwapo wataweza kuzungumza moja kwa moja kwa uwazi. 

Marekani yaonya dhidi ya ruzuku ya China kwa viwanda

Mkutano wao umefanyika baada ya Marekani na China kukubaliana kuwa na mazungumzo ya kina juu ya usawa katika ukuaji wa uchumi