1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanafunzi waliotekwa nyara Nigeria waokolewa

Zainab Aziz
25 Machi 2024

Jeshi na maafisa wa serikali nchini Nigeria wamesema zaidi ya watoto 130 waliotekwa nyara zaidi ya wiki mbili zilizopita kutoka kwenye shule yao katika jimbo la kaskazini-magharibi la Kaduna nchini Nigeria wameokolewa.

https://p.dw.com/p/4e6cG
Wanafunzi waliotekwa waachiwa huru, Nigeria
Wanafunzi waliotekwa na wanamgambo Al shabaab walioachiwa nchini NigeriaPicha: Ibrahim Yakubu/DW

Gavana wa Kaduna, Uba Sani ameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba ni vijana 137 walitekwa nyara wakati watu wenye silaha wanaoendesha pikipiki walipovamia shule ya Kuriga mnamo Machi 7.

Watekaji hawajalipwa kikomboleo kama walivyodai

Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja Jenerali Edward Buba, amesema katika watoto hao 137 waliokolewa katika jimbo la Zamfara, eneo lenye sifa za matukio ya utekaji nyara na ambalo liko umbali wa zaidi ya kilomita 200 kutoka shuleni kwao.