1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wabunge Sudan Kusini wamshutumu Kiir kukiuka makubaliano

Grace Kabogo
19 Septemba 2023

Kundi pinzani ndani ya bunge nchini Sudan Kusini limetoka bungeni, likimshutumu Rais Salva Kiir kwa kukiuka makubaliano tete ya amani, baada ya wenzao kupitisha muswada unaoruhusu uchaguzi kucheleweshwa.

https://p.dw.com/p/4WYn0
NO FLASH Sudan Referendum
Picha: picture alliance/dpa

Serikali ya umoja wa kitaifa kati ya Rais Kiir na mpinzani na makamu wake, Riek Machar, imeshindwa kutekeleza masharti kadhaa ya mkataba wa amani, ikiwemo kuandaa katiba na sheria ya uchaguzi kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

Soma zaidi: Sudan Kusini kuandaa uchaguzi wa kwanza wa rais 2024

Siku ya Jumatatu (Septemba 2023), wabunge wanaotoka katika chama cha Machar cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM) walipinga kupitishwa kwa Sheria ya Kitaifa ya Uchaguzi, wakionya kuwa ingelisababisha uchaguzi usio wa kidemokrasia, usio wa haki na usioaminika.

Wabunge hao walimshutumu Spika wa Bunge, Jemma Nunu Kumba, kwa kushinikiza kura hiyo bila kuwapa haki yao ya kutoa maoni kuhusu suala hilo muhimu.