Pembezoni mwa kongamano la nne la Idhaa za Kiswahili duniani lililofanyika Mbeya nchini Tanzania, Mohammed Khelef amezungumza na mtafiti wa lugha ya Kiswahili Daktari Nasra Habib wa chuo kikuu Huria cha Tanzania juu ya namna vyombo vya habari vinavyochangia kuharibu lugha ya Kiswahili.