1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

Von der Leyen: EU tayari kulinda uchumi wake dhidi ya China

6 Mei 2024

Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema muungano huo hautosita kuchukua hatua kali za kulinda uchumi wake na ulinzi, katikati mwa mivutano ya kibiashara na China.

https://p.dw.com/p/4fYMP
Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akizungumza na waandishi wa habari mjini Paris Mei 06, 2024.
Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen akizungumza na waandishi wa habari mjini Paris Mei 06, 2024.Picha: Dimitar Dilkoff/AFP

Von der Leyen ameyasema hayo mjini Paris kufuatia mazungumzo na Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

Kiongozi huyo wa ngazi ya juu ameeleza kwamba bado kuna tofauti baina ya Ulaya na China na ambazo zinazua wasiwasi mkubwa.

"Ili biashara iwe na usawa, ufikiaji wa soko la kila mmoja unapaswa kuwa wa pande zote. Na tumejadili namna ya kupiga hatua za kweli katika kulifikia soko. Bado nina imani kwamba maendeleo makubwa yanaweza kupatikana," amesema Von der Leyen.

Kando na Ufaransa, Rais Xi anatarajiwa pia kuzuru Serbia na Hungary.