1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi:NATO inazidi kujiingiza katika mzozo wa Ukraine

Amina Mjahid
14 Februari 2023

Bunge la Urusi limesema Jumuiya ya Kujihami NATO inayoongozwa na Marekani inaonyesha uadui wake dhidi ya Urusi kila siku, na inaendelea kujihusisha zaidi na mgogoro wa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4NTJn
Der russische Pressesprecher Dmitry Peskov
Picha: Elena Palm/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Msemaji wa bunge hilo la Kremlin, Dmitry Peskov, amewaambia waandishi habari kwamba NATO inatumia kila mbinu kuwa sehemu ya mzozo huo na hatua zaidi huenda zikachukuliwa kukomesha hilo.

Urusi iliwahi kusema kwamba silaha Ukraine inazopewa na mataifa wanachama wa NATO zinaurefusha mgogoro uliopo.

Soma pia:

Lakini Kiev na mataifa ya Magharibi zinasema msaada huo umelenga kuisadia Ukraine kujilinda dhidi ya mashambulizi ya jirani yake.

Mapema hii leo Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, alisema Jumuiya hiyo ni lazima ihakikishe Ukraine inapata silaha inazohitaji kushinda vita vyake na Urusi.