1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yawahamisha maelfu kutoka mji uliokumbwa na mafuriko

Sylvia Mwehozi
13 Aprili 2024

Mamlaka katika mji wa Orenburg nchini Urusi imetoa wito kwa maelfu ya wakaazi kuhama mara moja kutokana na kuongezeka kwa mafuriko baada ya kingo za mito mikubwa kupasuka kufuatia theluji inayoyeyuka.

https://p.dw.com/p/4eiPy
Urusi| Orenburg
Eneo la makazi likiwa limefurika maji mjini OrenburgPicha: Reuters

Mamlaka katika mji wa Orenburg nchini Urusi imetoa wito kwa maelfu ya wakaazi kuhama mara moja kutokana na kuongezeka kwa mafuriko baada ya kingo za mito mikubwa kupasuka kufuatia theluji inayoyeyuka.

Naibu meya wa mji wa Orenburg Alexei Kudinov, alisema hapo awali kwamba zaidi ya nyumba 360 na karibu mashamba 1,000 yalikuwa yamefurika maji usiku kucha.

Soma: Maelfu ya watu hatarini baada ya bwawa la Kakhovka kuripuliwa

Kiwango cha maji kinaripotiwa kuongezeka kwa kasi katika eneo jingine la Urusi la Kurgan na katika nchi jirani ya Kazakhstan. Hadi sasa watu takribani 100,000 wamehamishwa huku hali ya joto inayoongezeka ikizidi kuyeyusha theluji kubwa.

Kuongezeka kwa viwango vya maji pia kunatishia sehemu za kusini za Siberia Magharibi, bonde kubwa zaidi duniani la haidrokaboni na katika maeneo ya karibu na Mto mkubwa zaidi barani Ulaya wa Volga.