1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yarusha makombora, droni 23 kuelekea Ukraine

4 Desemba 2023

Jeshi la anga la Ukraine limesema Urusi ilirusha makombora ya masafa marefu na ndege 23 zisizo na rubani kuelekea maeneo mbalimbali ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4ZkYX
Mfumo wa kujilinda na makombora unaotumiwa na jeshi la Ukraine.
Mfumo wa kujilinda na makombora unaotumiwa na jeshi la Ukraine.Picha: Sebastian Christoph Gollnow/dpa

Jeshi hilo limeeleza kuwa mifumo yake ya ulinzi ilifanikiwa kuharibu makombora 18 kati ya hayo 23 kabla hayajafikia malengo yake.

Kupitia jukwaa la Telegram, jeshi la anga la Ukraine limesema mifumo ya ulinzi imewekwa katika mikoa karibu tisa nchini humo.

Hata hivyo, jeshi hilo la Ukraine halikutoa maelezo zaidi juu ya ndege zisizo na rubani ambazo hazikudunguliwa ama iwapo kuna uharibifu wowote uliotokana na shambulio hilo la Urusi.

Shirika la habari la Reuter limesema halikuweza kuthibitisha ripoti hiyo.