1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Urusi yakemea mashambulizi ya Marekani Iraq na Syria

6 Februari 2024

Urusi imekemea hatua ya Marekani ya kufanya mashambulizi katika mataifa ya Iraq na Syria.

https://p.dw.com/p/4c56C
Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa I Balozi wa Urusi Nebenzia
Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia Picha: Yuki Iwamura/AP/picture alliance

Moscow imesema hiyo ni mbinu ya rais Joe Biden ili kujipigia debe hasa wakati huu kampeni za uchaguzi zikipamba moto nchini humo, na kusisitiza kuwa mashambulizi hayo si majibu kwa wanajeshi wa Marekani waliouawa huko Jordan.

Katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi hayo na uliotishwa na Moscow, Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia amesema hakuna uhalali wowote wa hatua hiyo ya Marekani.

Soma pia: Iran yasema haitosita kujibu mashambulio yatakayoilenga nchi hiyo

Naibu Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema Marekani ina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya silaha kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Marekani iliazisha mkururo wa mashambulizi na kuyalenga makundi yenye mafungamano na Iran katika mataifa ya Iraq, Syria na Yemen na ilitangaza hivi majuzi kuwa inalenga kufanya mashambulizi zaidi kama hayo katika eneo la Mashariki ya Kati.