1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yaishutuju Ujerumani kwa "tabia ya uadui"

26 Januari 2024

Msemaji wa Rais Vladimir Putin wa Urusi, Dmitry Peskov, amesema Ikulu ya Kremlin inaishutumu Ujerumani kwa kile alichokiita "kuonesha tabia ya uadui."

https://p.dw.com/p/4bj4Q
 Kremlin, Dmitry Peskov
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov.Picha: Mikhail Tereshchenko/TASS/dpa/picture alliance

Kulingana na shirika la habari la Interfax, Peskov amesema kuwa si jambo la siri kwamba Ujerumani ipo kwenye mkondo wa makabiliano makali na Urusi.

Peskov pia amezungumzia juu ya mpango wa ulinzi wa Ujerumani kama jaribio la kuizuia Urusi.

Soma zaidi: UNHCR: Hali ya misaada ya kibinaadamu ni mbaya mno nchini Ukraine

Kamanda wa jeshi la Ujerumani, Luteni Jenerali Andre Bodemann, ameliambia shirika la habari la dpa mjini Berlin kuhusu mpango mpya wa utendaji kazi wa jeshi la Ujerumani, ambao unatoa taswira ya jinsi hatua za pamoja zinavyopaswa kuchuliwa iwapo kutatokea mvutano wa kikanda.

Msemaji huyo wa Kremlin ameongeza kuwa Urusi itauchunguza kwa kina mpango huo wa Ujerumani.

Peskov pia amekanusha ripoti kuwa Urusi imejitolea kwa njia isiyo rasmi kujadili na mataifa ya Magharibi namna ya kusitisha vita vyake nchini Ukraine.