1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuipatia Ukraine mfumo wa ziada wa ulinzi wa anga

13 Aprili 2024

Ujerumani imetangaza kwamba itaipatia Ukraine mfumo wa ulinzi wa anga wa nyongeza chapa Patriot ili kuiwezesha nchi hiyo kuongeza uwezo wake wa kudhibiti mashambulizi ya ndege za Urusi.

https://p.dw.com/p/4ejA3
Mfumo wa Ulinzi wa Anga aina ya Patriot
Mfumo wa Ulinzi wa Anga aina ya Patriot Picha: Mindaugas Kulbis/AP/picture alliance

Hayo yameelezwa hivi leo na wizara ya Ulinzi ya Ujerumani. Taarifa ya wizara hiyo imesema kutokana na kuongezeka kwa hujuma za anga za Urusi, serikali mjini Berlin imefikia uamuzi wa kuipiga jeki Ukraine kuimarisha uwezo wake wa kujilinda.

Uamuzi huo umetangazwa katika wakati mkuu wa majeshi wa Ukraine, Oleksandr Syrsky, amesema hii leo kwamba hali kwenye mstari wa mbele wa mapambano mashariki mwa nchi yake imezidi kuwa mbaya.

Kamanda huyo amesema hilo linatokana na kupamba moto kwa mashambulizi ya Urusi inayotumia silaha za kiwango cha juu. Utawala mjini Kyiv unalalamikia kucheleweshwa kwa msaada wa kijeshi kutoka mataifa ya Magharibi kama sababu ya hali hiyo.