1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yataka kubadilishana makombora na Ujerumani

Tatu Karema
25 Januari 2024

Uingereza imeitaka Ujerumani kubadilishana nayo makombora, hatua itakayoiwezesha serikali ya Ujerumani kupata njia ya kukabiliana na wasiwasi kuhusu pendekezo la usambazaji makombora kwa Ukraine

https://p.dw.com/p/4be5o
Picha iliyotolewa na jeshi la Ujerumani Bundeswehr  mnamo 28.03.2017 inaonyesha ndege ya kivita ya Tornado IDS ASSTA 3.0, ikiwa na kombora linaloongozwa na Taurus
Ndege ya kivita ya Tornado IDS ASSTA 3.0Picha: Andrea Bienert/Bundeswehr/dpa/picture alliance

Gazeti la Handelsblatt limenukuu vyanzo vya serikali na kidiplomasia vikisema kuwa wiki kadhaa zilizopita, serikali ya Uingereza ilikuwa imependekeza kwa Ujerumani kwamba inaweza kusafirisha makombora aina ya Storm Shadow kwa Ukraine,  na kwa upande wake, kupokea makombora aina ya Taurus ya Ujerumani.

Ofisi ya kansela wa Ujerumani yafanyia tathmini pendekezo

Ripoti hiyo imeongeza kuwa ofisi ya Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz imekuwa ikifanyia tathmini  pendekezo hilo.

Chanzo cha karibu na mazungumzo hayo, kimesema kuwa ubadilishanaji huo wa makombora unaopendekezwa huenda ukapata uungwaji mkono nchini Ujerumani.

Soma pia:Ukraine yasema ina uhakika Ujerumani itaipatia makombora ya Taurus

Hata hivyo serikali ya Ujerumani imekataa kutoa tamko lolote kuhusiana na ripoti hiyo.

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Uingereza, amesema kuwa nchi hiyo na washirika wake ikiwa ni pamoja na

Ujerumani zinaendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuipa Ukraine silaha bora kuiwezesha kutetea eneo lake.