1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yajiandaa kupeleka wanajeshi 1000 mashariki mwa Kongo

Saumu Mwasimba
24 Machi 2023

Uganda imesema itapeleka wanajeshi 1,000 katika eneo lenye machafuko la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mwezi huu kama sehemu ya kikosi cha kikanda.

https://p.dw.com/p/4PAPP
Demokratische Republik Kongo | Soldaten von Uganda und DRC | Archivbild
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Taarifa hiyo imetangazwa jana Alhamisi na afisa wa  jeshi la nchi hiyo, Kanali Mike Walaka  Hyeroba, aliyesema wanajeshi hao watapelekwa katika maeneo mbalimbali ya Kivu Kaskazini ambako hivi kunashikiliwa na waasi wa kundi la M23.

Burundi pia imepeleka pia wanajeshi wake katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini wa Goma wakati Sudan Kusini ikitangaza kwamba itapeleka kikosi chake cha wanajeshi 750 katika eneo hilo mwishoni mwa mwezi Desemba.

Soma pia: DRC: Mauaji dhidi ya raia yanaendelea licha ya uwepo wa vikosi vya usalama

Hatua hizo zinachukuliwa kama utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na nchi saba wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuleta uthabiti katika eneo hilo tete la Kongo.

Waasi wa M23 wameidhibiti sehemu kubwa ya mkoa wa Kivu Kaskazini tangu walipoanzisha tena harakati za uasi mwishoni mwa mwaka 2021 na kuwaacha maelfu ya Wakongomani bila makaazi.