1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak: Uingereza itasimama kidete na Ukraine

Sudi Mnette
3 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak aonesha dhamira ya dhati ya taifa lake kuisaidia Ukraine katika mapambano yake dhidi ya Urusi.Kauli hiyo ameitoa wakati wa mazungumzo ya simu na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

https://p.dw.com/p/4aoNp
London Premierminister Rishi Sunak | Familienvisa teurer
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak.Picha: James Manning/PA/dpa/picture alliance

Taarifa ya ofisi ya waziri mkuu huyo imesema Sunak ametoa ahadi ya msaada wa kijeshi na uungaji mkono wa kidiplomasia. Wakati wa mazungumzo yao ya simu, Sunak alitoa salamu za rambirambi kwa raia wote wa Ukraine waliouawa na kujeruhiwa katika mashambulizi ya kinyama ya anga ya Urusi katika kipindi cha Krismasi. Wiki iliyopita serikali ya Uingereza ilitangaza kuwa itatuma takriban makombora 200 ya ulinzi wa anga nchini Ukraine kutokana na hali ya mashambulizi ya hivi karibuni ya Urusi.