1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Urusi: Ukraine imeshambulia Zaporizhzhia na kuuwa watu 16

Lilian Mtono
14 Aprili 2024

Watu 16 wamekufa hadi sasa kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Ukraine katika mji wa Tokmak, katika mkoa wa Zaporizhzhia.

https://p.dw.com/p/4ejvK
Mashambulizi katika mkoa wa Zaporizhzhia
Waokoaji wa Urusi wa kikosi cha EMERCOM wakiondoa vifusi vya jengo la ghorofa kufuatia kushambuliwa kwa makombora ya Ukraine katika mji wa Tokmak katika mkoa wa Zaporizhzhia: 13.04.2024Picha: Yuri Voytkevich/Sputnik/SNA/IMAGO

Hayo yameelezwa leo na Afisa aliyeteuliwa na Urusi katika mkoa huo wa kusini mwa Ukraine Yevgeny Balitsky na kusisitiza kwamba watu 20 wamejeruhiwa kufuatia mashambulizi hayo ya usiku wa Ijumaa, na 12 wana hali mbaya.

Shirika la habari la Reuters hata hivyo halikuweza kuthibitisha taarifa hizi, na Ukraine haijasema chochote juu ya madai haya. Moscow na Kyiv wamekuwa wakituhumiana kufanya  mashambulizi eneo hilo.

Zaporizhzhia ni moja ya mikoa minne ya Ukraine iliyokuwa ikikaliwa kwa kiasi fulani na wanajeshi wa Urusi na ambayo Moscow iliyanyakua baada ya kuivamia kikamilifu Ukraine Februari mwaka 2022.