1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz aionya China kutoisaidia Urusi

Amina Mjahid
15 Aprili 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema atamuonya rais wa China Xi Jinping dhidi ya kutoa msaada wa kijeshi kwa Urusi.

https://p.dw.com/p/4eoIe
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Akizungumza mjini Shanghai, Scholz amesema atamueleza Xi kwamba Urusi inaendesha vita vya kuitwaa Ukraine na kusisitiza kwamba hakuna mtu anaepaswa kusaidia hilo kufanikiwa.

Ametoa wito pia wa kila mmoja kutokwepa vikwazo ilivyowekewa Urusi na pia kutaka nchi hiyo kutopewa silaha na nchi yoyote ile, akisema hilo pia linajumuisha bidhaa zinazoweza kutumiwa na raia pamoja na matumizi mengine ya kijeshi.

China ni mshirika mkubwa wa Urusi na inadaiwa kutoa silaha kwa taifa hilo lililo vitani na nchi jirani ya Ukraine.

Kansela huyo wa Ujerumani amesema vita vya Urusi nchini Ukraine sio tatizo la Ulaya pekee, ni mzozo ambao ukitanuka zaidi utatoa kitisho kikubwa cha usalama duniani.  Scholz atakutana kesho Jumanne na Xi Jinping na Waziri Mkuu  Li Qiang mjini Beijing.