1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Vladmir Putin amempokea rais wa Syria Bashar al-Assad

Bruce Amani
15 Machi 2023

Rais wa Urusi Vladmir Putin amempokea hii leo rais wa Syria Bashar al-Assad kwa mazungumzo, wakati Kremlin ikiongeza juhudi za usuluhishi kati ya Uturuki na mshirika wa Moscow Damascus.

https://p.dw.com/p/4Oife
Russland, Moskau | Syriens Präsident Assad in Russland
Picha: SANA/dpa/picture alliance

Kusaidia kurejesha uhusiano kati ya Uturuki na Syria kunatoa fursa kwa Kremlin kujiimarisha kidiplomasia, wakati ambapo Moscow inazidi kutengwa na mataifa ya magharibi baada ya kutuma vikosi vyake kuivamia Ukraine.

Mkutano huo unafuatia tangazo la wiki iliyopita la urejeshaji wa uhusiano kati ya mahasimu wa Mashariki ya Kati, Saudi Arabia na Iran, ulioratibiwa na China.

Soma pia:Putin ampongeza Xi kwa kuongezewa muhula wa tatu madarakani

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kuwa mkutano kati ya Putin na Assad, aliewasili Moscow jana Jumanne jioni, unaangazia uhusiano kati ya mataifa hayo, lakini pia uhusiano kati ya Uturuki na Syria utagushwa kwa njia moja au nyingine.