1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin anaimani na mipango ya operesheni dhidi ya Ukraine

25 Juni 2023

Rais Vladmir Putin amesema kuwa yuko kwenye mawasiliano ya kila wakati na wizara ya ulinzi ya Urusi na kuwa nchi yake ina imani ya kufanikisha mipango yake inayohusu operesheni maalumu nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4T2as
Russland | TV Ansprache Putin
Picha: via REUTERS

Putin ameyasema hayo katika mahojiano aliyoyafanya mapema leo na mwandishi wa ikulu ya Kremlin Pavel Zarubin  kupitia televisheni ya Rossiya ya Urusi.

Soma pia: Rais wa Urusi Vladimir Putin asema uasi wa mamluki wa Wagner ni usaliti.

Wakati huo huo, Korea Kaskazini imesema kuwa inaiunga mkono Urusi katika kukabiliana na uasi wa kundi la mamluki la Wergner. Haya ni kwa mujibu wa shirika la serikali la habari la Korea Kaskazini(KCNA).

Katika mkutano wake na balozi wa Urusi huko Pyongyang Alexander Matsegora, naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Im Chon Il alionyesha imani thabiti kwamba uasi wa hivi karibuni nchini Urusi utakomeshwa.

Soma pia: Putin amtuhumu Prigozhin na kundi lake kwa usaliti

Huu ni ujumbe wa hivi karibuni wa uungwaji mkono kutoka Korea Kaskazini kwa Moscow tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, ambavyo Urusi imevitaja kama "vita vinachochewa na nchi za magharibi " vyenye nia ya kuiangamiza.