1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Obi kupinga mahakamani matokeo ya uchaguzi Nigeria

1 Machi 2023

Chama cha Labour nchini Nigeria kinachoongozwa na mgombea wa urais Peter Obi kitawasilisha kesi mahakamani kupinga kuchaguliwa kwa rais mteule Bola Tinubu

https://p.dw.com/p/4O7h4
Nigeria | Präsidentschafts- und Parlamentswahlen
Picha: Patrick Meinhardt/AFP

Haya ni kulingana na mgombea mwenza wa Obi. Haya yanafanyika baada ya Tinubu kutangazwa na Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi nchini humo INEC kuwa mshindi wa kura ya urais.

Tinubu wa chama tawala cha All Progressives Congress APC amepata jumla ya kura milioni 8.8 huku mpinzani wake Atiku Abubakar akipata kura milioni 6.9.

Soma pia:Baada ya kushinda urais, Tinubu ahimiza mshikamano Nigeria

Tinubu sasa anachukua nafasi ya Muhammadu Buhari ambaye anaachia ngazi baada ya kuhudumu kwa mihula miwili. Wanigeria walikuwa wanatarajia kupata rais atakayekuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazozidi za kiusalama, kiuchumi na kupunguza umaskini.