1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Palestina: Hospitali ya kuhamishika imewasili Gaza

Amina Mjahid
20 Novemba 2023

Maafisa wa Palestina wamesema, hospitali ya kuhamishwa iliyotumwa huko na Jordan imefikishwa katika Ukanda wa Gaza leo Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4ZEfa
Ukanda wa Gaza | Mhudumu akimnywesha mtoto mchanga maziwa
Afya | Mhudumu wa afya akimuhudumia mtoto njiti alieokolewa kutoka hospitali ya Al Schifa.Picha: Rizek Abdeljawad/Xinhua/picture alliance

Hospitali hiyo ni ya kwanza tangu kuanza kwa vita kati ya Israel na watawala wa eneo hilo wa Hamas mnamo Oktoba 7.

Mohammed Zaqout, Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Gaza amesema hospitali hiyo itawekwa katika mji wa Khan Yunis, ili kuwapokea wagonjwa na wale waliojeruhiwa kufuatia hali mbaya inayoshuhudiwa katika hospitali za Kusini mwa Gaza, huku mamia ya waliojeruhiwa wakiongezeka kila siku kufuatia mashambulizi ya angani kutoka Israel. 

Soma pia:China yatoa mwito kuzuwia kueneo mgogoro wa kibinadamu Gaza

Kulingana na wizara ya Afya ya Gaza, jumla ya watu 30,000 wamejeruhiwa katika ukanda huo.

Watu waliouwawa tangu kuanza kwa vita hivyo wamefikia zaidi ya 13,000 wengi wao wakiwa raia.