1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Mshambuliaji ajitoa mhanga katikati mwa mji mkuu wa Uturuki

1 Oktoba 2023

Mshambuliaji mmoja wa kujitoa mhanga amejilipua katikati mwa mji mkuu wa Uturuki, Ankara, hii leo, saa chache kabla ya kuanza tena kwa vikao vya Bunge baada ya mapumziko ya msimu wa kiangazi.

https://p.dw.com/p/4X15d
Ankara, Uturuki
Watoa huduma za dharura wakiwa eneo la mkasa mjini AnkaraPicha: Alican Uludag/DW

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Ali Yerlikaya amearifu juu ya kisa hicho kupitia mitandao ya kijamii akisema mshambuliaji aliyevaa mkanda wa mabomu alijilipua kwenye lango la ofisi ya wizara yake. Amesema polisi ilimpiga risasi mshambuliaji wa pili na kumuua.

Shambulizi hilo limetokea kwenye eneo lenye ofisi nyingi za serikali na majengo ya Bunge ikiwa ni muda mfupi kabla ya rais Recip Tayyip Erdogan kutoa hotuba ya kufungua vikao vya bunge baada ya miezi mitatu ya mapumziko.

Hadi sasa bado hakuna taarifa juu ya washambulizi lakini katika miaka ya karibu wapiganaji wa jamii ya kikurdi na wanamgambo wa itikadi kali wamekua wakiilenga Uturuki kwa mashambulizi ya kuvizia.