1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Misaada yashindwa kufikishwa maeneo ya mafuriko Afghanistan

Tatu Karema
12 Mei 2024

Vikosi vya kutoa msaada wa dharura na uokoaji vimetatizika kufika maeneo ya kaskazini mwa Afghanistan yaliyoathirika na mafuriko yaliosababisha vifo vya mamia ya watu

https://p.dw.com/p/4flDF
Mto uliofurika nchini Afghanistan baada ya kunyesha kwa mvua kubwa mnamo Mei 10, 2024
Mafuriko nchini AfghanistanPicha: AFP

Katika eneo la Sheikh Jalal, mojawapo ya maeneo yaliyoharibiwa zaidi, AFP imeelezea kuhusu malori ya misaada yaliojaa chakula, magari ya kijeshi, maafisa wa uokoaji na wakaazi wa eneo hilo wakiwa wamekwama katika maeneo ambayo barabara zilikuwa zimesombwa kabisa.

Soma pia:WFP: Mvua imesababisha vifo vya watu 300 Afghanistan

Mohammad Ali Aryanfar, mmoja wa maafisa wa shirika la Uturuki la kutoa msaada wa kibinadamu la Hak linalojaribu kupeleka chakula katika eneo la Burka, amesema wamekuwa barabarani tangu mapema leo lakini wamekwama katika eneo la Sheikh Jalal.

WFP yatumia njia mbadala kufikisha msaada katika maeneo yalioathirika

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani - WFP, lilituma picha kwenye mtandao wa kijamii wa X likionesha mifuko ya unga ikiwa imefungwa kwenye migongo ya punda, na kusema iliwabidi kutafuta njia mbadala ili kufikisha chakula hicho kwa manusura wa mafuriko hayo huko Baghlan.