1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Miripuko yailenga ghala la maroketi nchini Syria

Bruce Amani
13 Agosti 2023

Shirika la habari la Syria linalomilikiwa na serikali SANA limeripoti kuwa milio ya milipuko ilisikika alfajiri ya Jumapili kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Damascus

https://p.dw.com/p/4V7Jx
Syrien Damaskus Explosionen im Osten der Stadt
Picha: Muhammad Khair/AA/abaca/picture alliance

Limelinukuu shirika la haki za binadamu linalofuatilia habari za vita likisema kuwa milipuko hiyo ililenga na kuharibu ghala la kuhifadhi roketi llinalomilikiwa na makundi yanayoiunga mkono serikali ya Iran.

Soma pia: Watu wenye silaha waua askari 23 Syria

Tukio hilo linafuatia shambulio jingine la anga la Jumatatu iliyopita lililofanywa na Israel karibu na Damascus. Wanajeshi wanne wa Syria na wapiganaji wawili wanaoiunga mkono serikali ya Iran waliuwawa kwenye shambulio hilo.

Iran imekuwa mshirika mkubwa wa Rais Bashar al Assad katika miaka 12 ya mzozo wa Syria. Wapiganaji ambao ni mawakala wa Iran kwenye vita hivyo, kundi la Hezbollah la Lebanon ma makundi ya Iraq yanayoiunga mkonono Tehran yanashikilia sehemu kubwa za mashariki, kusini na kaskazini mwa Syria pamoja na vitongoji vinavyouzunguka mji mkuu.