1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Mfalme Charles kuzuru Ujerumani na Ufaransa

3 Machi 2023

Kasri la Buckingham limetangaza Ijumaa kuwa Mfalme Charles wa III wa Uingereza atafanya ziara yake ya kwanza ya kiserikali kuelekea Ufaransa na Ujerumani baadaye mwezi huu.

https://p.dw.com/p/4OEJ7
König Charles III.
Picha: Aaron Chown/Pool PA/AP/dpa/picture alliance

Chaguo la kuanza kuyatembelea mataifa hayo ambayo pia ni washirika wake wa karibu, linatazamiwa kama jaribio la kufufua uhusiano baada ya Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya katika kile kinachofahamika zaidi kama "Brexit".

Ziara ya Mfalme Charles wa III atakayeambatana na mkewe Camilla, itaanza Machi 26 hadi 31, kabla ya sherehe za kutawazwa rasmi Ufalme zitakazofanyika Mei 6 mwaka huu. Charles wa III atapokewa nchini Ufaransa na rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron.