1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ni hafifu kuhusu usitishwaji mapigano huko Gaza

5 Mei 2024

Mazungumzo yanayolenga kufikiwa makubaliano ya usitishwaji mapigano huko Gaza yanatarajiwa kuanza tena siku ya Jumapili mjini Cairo nchini Misri lakini pande zote zimeshindwa kuafikiana juu ya maswala muhimu.

https://p.dw.com/p/4fWCO
Cairo | Rais Abdel Fattah el-Sisi akizungumza na Mkuu wa CIA William J. Burns
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi (katikati) akifanya mazungumzo na Ujumbe kutoka Marekani kufutia vita vya GazaPicha: Presidency of Egypt/Handout/Anadolu/picture alliance

Matarajio ya kufikiwa kwa makubaliano ya usitishwaji mapigano katika vita vya Gaza yameonekana kuwa hafifu wakati wa mazungumzo mengine ya upatanishi mjini Cairo nchini Misri. 

Kundi la Hamas limekataa makubaliano yoyote ambayo hayatohusisha kumalizika kabisa kwa vita na wanajeshi wa Israel kuondoka katika ardhi ya Palestina. Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kamwe hawatokubaliana na matakwa hayo.

Wapatanishi kutoka Qatar, Misri na Marekani wanadhamiria kufikia makubaliano yatakayo vimaliza vita hivyo vilivyodumu kwa miezi saba, na wamependekeza kusitishwa kwa mapigano kwa muda wa siku 40 na kubadilishana mateka pamoja na wafungwa wa Kipalestina.

Soma pia: Misri ina matumaini kuwa Israel, Hamas watafikia makubaliano

Pande zote mbili wametupiana lawama kwa kukwamisha mazungumzo hayo huku Kiongozi Mkuu wa Kundi la Hamas Ismail Haniyeh akimtuhumu Netanyahu kwa kuhujumu juhudi za wapatanishi.