1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mawaziri wa NATO wajadili ufadhili wa kifedha kwa Ukraine

3 Aprili 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo wamejadiliana kuhusiana na kubuniwa kwa mfuko wa yuro bilioni 100 kwa ajili ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4eOn8
Frankreich La Celle Saint-Cloud | Außenminister-Treffen des Weimarer Dreiecks
Picha: Sarah Meyssonnier/AP/dpa/picture alliance

Mawaziri wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo wamejadiliana kuhusiana na kubuniwa kwa mfuko wa yuro bilioni 100 kwa ajili ya Ukraine.

Akizungumza mjini Brussels kunakofanyika kikao hicho, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg, amewataka mawaziri hao wahakikishe jeshi la Ukraine linapata usambazaji wa muda mrefu wa silaha.

Maafisa wanasema, pendekezo hilo la mfuko wa yuro bilioni 100 limetolewa na Stoltenberg kama tahadhari ya uwezekano wa Donald Trump kurudi ofisini kama rais wa Marekani baada ya uchaguzi wa Novemba.

Mpango huo umeungwa mkono na wandani wakubwa wa Ukraine kama Poland na mataifa ya Baltiki. Lakini wengine wanatahadharisha kuhusiana na ufadhili utakakotokea na kwamba mpango huo unaweza kubadilika pakubwa, ifikapo mwezi Julai pale jumuiya hiyo ya NATO itakapofanya mkutano wake mwengine wa kilele mjini Washington.