1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yakabiliwa na kitisho cha wimbi la joto kali

Sudi Mnette
14 Juni 2022

Wamarekani zaidi ya milioni 100 wametahadharishwa kusalia majumbani mwao, Kutokana na kitisho cha hali mbaya ya joto kali na fukuto katika maeneo ya majimbo ya Pwani ya Ghuba, Maziwa Makuu na mashariki mwa Carolina.

https://p.dw.com/p/4CeLx
USA Hitzewelle
Picha: Ted S. Warren/AP/picture alliance

Kituo cha Utabiri wa Huduma ya Hali ya Hewa ya Kitaifa cha huko, Maryland kimesema hadi Juamatano watu milioni 107.5 wanaweza kuathiriwa na kadhia inayojumuisha mchanganyiko hali ya joto katika maeneo hayo.

Kituo cha taifa cha huduma ya hali ya hewa kimesema kwa mwisho wa juma wimbi la joto, ambalo tayari limeainisha rekodi kadhaa za juu katika maeneo ya Magharibi, Kusini Magharibi na hadi mjini Denver na linatarajiwa kuenea katika maeneo ya Maziwa Makuu hadi Mashariki mwa Carolina.

Kiwango cha ongezeko la joto kufikia nyuzi joto 43.

USA HItzewelle in Kalifornien | Whitewater River, Kühlung
Raia wa Marekani wakikabiliana na ongezeko la jotoPicha: Mario Tama/Getty Images

St Louis, Memphis, Minneapolis na Tulsa ni miongoni mwa miji kadhaa iliyo chini ya maonyo ya joto kupita kiasi, pamoja na utabiri wa halijoto kufikia nyuzi joto 38, ikifuatana na unyevu wa juu ambao unaweza kufanya hali ya fukuto kufikia kiwango cha nyuzi joto 43.

Katika eneo moja jimboni Mississipi mapema Jumatatu, wakazi walikabiliwa na kiwango cha joto kilichofikia nyuzi joto 35. Manispaa nyingi nchini Marekani zimetangaza vituo vya kupoza joto, likiwemo jiji la Chicago, eneo ambalo jana Jumatatu maafisa walishuhudiwa wakiwatahadharisha wakazi, kwamba ipo fursa ya kupata unafaa kwa nyenzo zilizopo kutokana na kitisho cha joto hilo.

Mamlaka zimeanza kutenga maeneo ya kujipoza na joto.

Mpango ya jiji hilo ni kufungua vituo sita leo na kesho vya kusaidia jamii katika kukabiliana na wimbi la joto na kwamba pia watu wanaweza kwenda kupata nafuu hiyo katika maktaba za umma za jiji hilo. Jiji liliongeza juhudi za kukabiliana na mawimbi ya joto baada ya zaidi zaidi ya watu 700, wengi wao wakiwa wazee, kupoteza maisha katika wimbi la joto la 1995.

Na mashaka zaidi yaliongezeka baada ya wanawake watatu kufariki katika nyumba ya kuwahifadhi wazee baaada ya kutokea ongezeko la muda mfupi la kiwango cha joto mwezi uliopita, na kuongeza wasiwasi kuhusu uwezo wa jiji  katika kukabiliana na wimbi la joto kali.

Katika eneo la Mecklenburg huko jimboni North Carolina serikali ya mtaa ilifungua vituo vya raia kujipoza na joto na kumewkwa pia fursa ya usafiri wa bure kwa baadhi ya maeneo. Juhudi kama hizo zinafanyika katika majimbo mengene kama Minneapolisi, ambako shule 14 ambazo hazina vipoza joto au viyoyozi zitafungwa na wanafunmzi kuendelea na masomo kwa njia ya mtandao kuanzia leo hii.

Soma zaidi: IPCC:kutoa ripoti ya hali ya joto duniani

Hali kama hiyo ilitokea mwaka jana, ambapo joto lilizilazimisha baadhi ya shule kuendelea na masomo kwa njia ya mtandao katika siku tatu katika siku za mwisho za masomo.

Chanzo: APE