1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuhimiza ufadhili wa Jumuiya ya kimataifa kwa Sudan

Bruce Amani
11 Aprili 2024

Marekani itaihimiza Jumuiya ya kimataifa kuchangisha zaidi ya dola milioni moja katika ufadhili wa ziada ili kukabiliana na mgogoro wa Sudan.

https://p.dw.com/p/4eevO
Sudan | die Generäle Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan und Mohamed Hamdan Dagalo
Kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al Burhan na kiongozi wa wanamgambo wa RSF Mohammad DagaloPicha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan Thomas Perriello amesema Washington itawashinikiza washiriki katika mkutano wa wafadhili kuhusu mzozo huo wa kibinaadamu utakaoandaliwa mwezi huu.

Mjumbe huyo amesema anatumai washirika kote duniani watavipa kipaumbele vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan na kwamba nchi zaidi zitajitokeza katika kongamano la wafadhili mjini Paris Jumatatu ijayo.

Aprili 15 itakuwa ni mwaka mmoja tangu mzozo huo kuzuka baada ya mvutano wa muda mrefu kuzuka na kusababisha mapigano makali kati ya jeshi na kikosi cha Rapid Support Forces (RSF).