1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Urusi yaishambulia bandari ya odesa nchini Ukraine

25 Septemba 2023

Urusi imefanya mashambulizi ya makombora usiku wa kuamkia leo katika bandari ya kusini mwa Ukraine ya Odessa na kumjeruhi mtu mmoja na kuharibu ghala la nafaka

https://p.dw.com/p/4WlXe
Hoteli iliyoharibiwa na shambulio la Urusi jimboni Odessa nchini Ukraine mnamo Septemba 25, 2023
Hoteli iliyoharibiwa na shambulio la Urusi jimboni OdessaPicha: State Emergency Service of Ukraine/REUTERS

Jeshi la Ukraine limesema kuwa mifumo yake ya ulinzi wa anga imeharibu ndege zisizo na rubani za Urusi zipatazo 19 za Shahed zilizotengenezwa na Iran, makombora 13 ambayo mawili ni ya masafa marefu. Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema pia imeharibu droni za Ukraine katika rasi ya Crimea.

Soma pia:Urusi yafanya mashambulio ya Droni katika mji Odessa

Hali ya mkoa wa Odessa pamoja na bandari zake imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu baada ya Ukraine kutangaza kutumia ukanda salama wa baharini ili kusafirisha nafaka kupitia Bahari Nyeusi, licha ya Urusi kujiondoa mwezi Julai katika mkataba wa kimataifa wa usafirishaji nafaka.