1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwa muda gani Netanyahu ataendelea kubakia tena madarakani?

Mohammed Khelef
4 Aprili 2024

Maelfu ya waandamanaji wa Israel wanaingia mitaani wakimtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ajiuzulu na wengi wanastaajabu ni kwa muda gani mwanasiasa huyo ataweza kuendelea kusalimika na kusalia madarakani.

https://p.dw.com/p/4ePrU
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, anakabiliwa na shinikizo kubwa kutoka ndani ya nchi yake.Picha: Maya Alleruzzo/AP/dpa/picture alliance

Netanyahu, mwenye uhakika na matumaini ya kuchaguliwa tena, anaonekana kuwa dhaifu kimwili na kisiasa. Sio maarufu sana, si zaidi ya asilimia nne ya Waisraeli wanamuamini. Hiyo ni kulingana na utafiti wa maoni uliofanywa mwaka uliopita, huku vita vya Gaza vikimsababishia madhara mtu ambaye Waisraeli wanamuita Bibi.

Wakati wa hotuba iliyotolewa kwenye televisheni siku ya Jumamosi na waziri wake wa zamani na mwanachama mwenzake wa chama cha Likud, Limor Livnat, ambaye aliviita vita vya Gaza kuwa "janga", Netanyahu alionekana kuwa dhaifu na mwenye utulivu, akiwa na hasira na kuchanganyikiwa.

Soma zaidi: Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lashindwa kupitisha azimio la kusitisha mapigano Gaza

Gazeti la kila siku la Haaretz, lenye kufuata siasa za mrengo wa kushoto, liliandika kuwa Netanyahu alionekana "kama mbabe aliyeogopa".

Netanyahu alionekana kudhoofika zaidi wakati alipoondoka hospitali mjini Jerusalem, siku ya Jumanne baada ya kufanyiwa upasuaji wa ngiri na kukabiliwa na ukosoaji wa jumuia ya kimataifa, baada ya wafanyakazi saba wa shirika la kutoa misaada lenye makaazi yake nchini Marekani walipouawa kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Mzimu unaofufuka kila unapozikwa

Emmanuel Navon, mwanachama wa zamani wa Likud na profesa wa sayansi ya siasa, anasema mara nyingi huko nyuma Nenyatahu amekuwa akizikwa kisiasa na akarejea tena.

Hata hivyo, Navon anasema wakati huu ni tofauti kwa sababu ya shambulizi la Oktoba 7.

Idadi ya vifo na majeruhi yaongezeka Ukanda wa Gaza

"Sio Israel ya zamani tena. Ni mwisho wa Bibi", anasema profesa huyo akiongeza kuwa Netanyahu mwenye umri wa miaka 76 hafanyi mazoezi yoyote, ana kazi ngumu sana, na aliwekewa kifaa cha kumsaidia kufatilia mwenendo wa mapigo ya moyo miezi sita iliyopita.

Soma zaidi: Netanyahu aapa kuendelea na vita licha ya shinikizo la kimataifa

Hata hivyo, mchambuzi Navon ana wasiwasi kuwa Netanyahu atalazimika kuondoka madarakani kutokana na wimbi jipya la maandamano makubwa, achilia mbali hasira za familia za watu wanaoshikiliwa mateka.

Einav Zangauker, mama wa mmoja wa watu 134 ambao bado wanashikiliwa mateka huko Gaza, amempachika Netanyahu jina la "firauni, muuaji wa watoto wa kwanza kuzaliwa."

Maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem.
Maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem.Picha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Matamshi hayo aliyatoa wakati wa maandamano ya usiku wa Jumanne (Aprili 2) nje ya jengo la bunge mjini Jerusalem, ukiwa ni usiku wa nne mfululizo wa maandamano.

Familia za watu wanaoshikiliwa mateka wameungana na waandamanaji wanaoipinga serikali ambao walitumia miezi tisa kuingia mitaani mwaka uliopita wakijaribu kuzuia mageuzi yenye utata ya mahakama yaliyoshinikizwa na washirika wa Netanyahau wenye kufuata siasa kali za mrengo wa kulia.

Maadui waongezeka

Huku muungano wake ukiyumba kutoka kwenye mgogoro mmoja hadi mwingine, maadui wanaonekana kuongezeka kuliko wakati mwingine wowote kumzungukaNetanyahu.

Waendesha mashtaka wanaendelea na kesi ya ufisadi dhidi yake licha ya vita, na waandamanaji walijaribu kuvunja vizuizi vya polisi kufika nyumbani kwake siku ya Jumanne kwa mara ya pili ndani ya siku nne.

Hata waziri wake wa ulinzi, Yoav Gallant, amekuwa akimpinga kuhusu suala lenye mgawanyiko mkubwa la Wayahudi wenye imani kali ya Kiorthodox kukwepa kuhudumu jeshini hata wakati vita vikiendelea kwenye Ukanda wa Gaza na vita vyengine vikinyemelea kati ya Israel na kundi la Hizbullah linaloungwa mkono na Iran nchini Lebanon.

Maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem.
Maandamano dhidi ya Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem.Picha: Ronen Zvulun/REUTERS

Soma zaidi: Biden kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu

Kwa muda mrefu Netanyahu amekuwa akitegemea kuungwa mkono na vyama vya kidini ili aweze kutawala.

Jenerali Reuven Benkler anasema mateka hawatorudi nyumbani wakati Bibi bado yuko madarakani.

Anasema Netanyahu amekuwa akiendeleza vita huko Gaza ili kurefusha utawala wake, madai ambayo yamerudiwa mara kwa mara kwenye maandamano.

Mchambuzi Navon anasisitiza kuwa Netanyahu hajali kuhusu mtu mwingine yeyote, isipokuwa yeye mwenyewe, na kwamba Netanyahu amefanikiwa kuwepo katika siasa za Israel kwa miongo mitatu kutokana na kuwagawa na kuwatala wananchi.

Na madai yake kwamba yeye pekee ndiye angeweza kuiweka nchi salama, yalisambaratishwa Oktoba 7.

/AFP