1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya, Ujerumani kuondowa vikwazo vya ushuru

Mohammed Khelef
28 Machi 2023

Kenya na Ujerumani zimekubaliana kutowa kipaumbele katika kuondowa vizuizi visivyohusiana na ushuru, kupunguza gharama za kibiashara na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4PMsW
Berlin | Bundespräsident Frank Walter Steinmeier trifft mit Kenias Präsident William Ruto
Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Hatua hiyo itatoa fursa ya kuimarishwa  uwekezaji wa makampuni ya Ujerumani nchini Kenya na kuboresha uwiano wa kibiashara ambao kwa sasa unaipendelea Ujerumani.

Rais wa Kenya  William Ruto ambaye hapo jana alifanya mazungumzo na Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier mjini Berlin amesema nchi hizo mbili zimekubaliana kuunda ushirikiano wa kina na mpana wa kiuchumi kwa ajili ya ustawi wa pande zote mbili.