1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kasisi aliyeongoza ibada ya mazishi ya Navalny aadhibiwa

24 Aprili 2024

Kanisa la madhehebu ya Orthodox la Urusi limemuadhibu kasisi aliyeongoza ibada ya mazishi ya kiongozi mkuu wa upinzani Alexei Navalny

https://p.dw.com/p/4f9CC
Alexei Nawalny
Aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa upinzani nchini Urusi hayati Alexei NavalnyPicha: Vuk Valcic/ZUMAPRESS/picture alliance

Vyombo vya habari vya Urusi, vimenukuu askofu wa mkuu wa kanisa hilo, Kwamba Kasisi Dmitry Safronov amepigwa marufuku kuongoza ibada kwa miaka mitatu ijayo, haruhusiwi tena kutoa baraka, kuvaa vazi la ukuhani na amepigwa marufuku kuongoza shughuli za uchungaji Moscow. 

Badala yake, kasisi huyo sasa atafanya kazi ya kutoa msaada kwa makuhani kama mwimbaji wa zaburi katika kanisa jengine, na 
hatima yake kama kasisi itaamuliwa kwa msingi wa tathmini ya kazi yake mpya.

Navalny azikwa mjini Moscow

Safronov aliongoza ibada ya mazishi kwenye kaburi la Navalny kwa siku 40 baada ya kifo chake kulingana na muongozo wa Kanisa la Orthodox, la kuwakumbuka marehemu siku ya 3, 9 na 40 baada ya kifo chao.