1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kashfa ya rushwa yamng´oa Spika wa Bunge la Afrika Kusini

4 Aprili 2024

Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake pamoja na kiti cha ubunge siku moja baada ya mahakama kutupilia mbali ombi lake la kuzuia kukamatwa kwa tuhuma za ufisadi.

https://p.dw.com/p/4ePGU
 Nosiviwe Mapisa-Nqakula
Aliyekuwa Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula.Picha: RODGER BOSCH/AFP

Kwenye barua yake ya kujiuzulu Bibi Nqakula amesema anataka kutumia muda wake kushughulikia uchunguzi ulioanzishwa dhidi yake.

Anatuhumiwa kupokea hongo ya dola 135,000 kutoka kwa mkandarasi mmoja wakati alipokuwa waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini. Inaelezwa kwamba alipatiwa kitita hicho kati ya Disemba 2016 na Julai 2019 na fedha nyingine ya rushwa ya zaidi ya kiasi dola 100,000 hazikulipwa.

Mwenyewe anakanusha madai hayo na amesema uamuzi wake wa kujiuzulu haumaanishi kwamba anakiri mashtaka yanayomwandama.