1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMali

Kamanda wa IS auwawa nchini Mali

Amina Mjahid
1 Mei 2024

Serikali ya Mali imesema kamanda mkuu wa kundi la dola la kiislamu aliyekuwa anatafutwa kufuatia kuhusika kwake na moja ya mashambulizi mabaya zaidi ya wanajeshi wa Marekani barani Afrika ameuwawa.

https://p.dw.com/p/4fOda
Kundi la wapiganaji wa Azawad nchini Mali
Kundi la wapiganaji wa Azawad nchini MaliPicha: Souleymane Ag Anara/AFP

Awali Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani ilitangaza zawadi ya dola milioni 5 kwa mtu yoyote aliyekuwa na habari kuhusu miendendo yake. Huzeifa  anaaminika kusaidia kupanga mashambulizi yaliyotokea mwaka 2017 kwa wanajeshi wa Marekani na Nigeria katika eneo la Tongo Tongo, nchini Niger. wanajeshi wannne wa nchi zote mbili waliuwawa katika shambulizi hilo.

Kufuatia shambulizi hilo, jeshi la Marekani lilisogeza nyuma operesheni zake na washirika wake katika eneo la sahel.