1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yashambulia Gaza huku vita vikikaribia siku 100

13 Januari 2024

Israel imeyapiga maeneo ya Gaza Jumamosi wakati Ukanda huo wa Kipalestina ukikabiliwa na hali ngumu ya kibinaadamu na kukumbwa na tatizo la kukatika mawasiliano ya simu katika siku ya 99 ya vita

https://p.dw.com/p/4bCK6
Vita kati ya Israel na Hamas vimetimiza siku 100
Makombora ya Israel yanaendelea kuyapiga maeneo ya Ukanda wa GazaPicha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Israel imeyapiga maeneo ya Gaza Jumamosi wakati Ukanda huo wa Kipalestina ukikabiliwa na hali ngumu ya kibinaadamu na kukumbwa na tatizo la kukatika mawasiliano ya simu katika siku ya 99 ya vita.

Soma pia: Israel yaiataka mahakama ya ICJ kutupilia mbali kesi dhidi yake

Mashuhuda wamesema Israel ilifanya mashambulizi Gaza mapema leo asubuhi, naye mwandishi habari wa AFP akisema makombora yaliyapiga maeneo kati ya miji ya kusini mwa Gaza ya Khan Yunis na Rafah, ambayo yamefurika watu waliokimbia kutoka kaskazini mwa Gaza.

Soma pia:Israel: Kesi ya mauaji ya Kimbari haina hoja za msingi 

Huduma zote za intanet na mawasiliano ya simu zilikatizwa Ijumaa kufuatia mashambulizi hayo ya Israel, kwa mujibu wa kampuni kuu ya mawasiliano ya eneo hilo Paltel. Shirika la Misaada ya Kiutu la Umoja wa Mataifa OCHA limesema Israel inaendelea kuzuia misafara inayopeleka misaada ya kiutu kaskazini mwa Gaza.

Hofu ya mgogoro huo kusambaa imeongezeka baada ya wanajeshi wa Marekani na Uingereza kuwashambulia waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoliunga mkono kundi la Hamas kufuatia mashambulizi yao kwenye meli zinazotumia Bahari ya Shamu.