1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yakubali pendekezo la wapalestina kurejea Gaza

Tatu Karema
10 Aprili 2024

Israel imekubali mpango wa kuwaruhusu wapalestina kurejea katika eneo la Kaskazini mwa Ukanda wa Gaza wakati wa mazungumzo ya kusitisha mapigano nchini Misri

https://p.dw.com/p/4edUy
Israel | Benjamin Netanjahu
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Ohad Zwigenberg/AFP/Getty Images

Maafisa wawili wanaofahamu kuhusu mazungumzo hayo, wamesema chini ya pendekezo la Marekani la kusitisha mapigano, Israel itaruhusu kurejea kwa Wapalestina 150,000 kaskazini mwa Gaza bila ukaguzi wa kiusalama.

Kwa upande wake, Hamas itahitajika kutoa orodha ya mateka wanawake, wazee na wagonjwa inaowashikilia.

Biden: Sikubaliani na mbinu za Netanyahu huko Gaza

Ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ilikataa kutoa maoni kuhusu suala hilo.

Hapo jana, kundi la Hamas lilisema kuwa pendekezo la hivi karibuni zaidi lililotolewa na wapatanishi wa Misri na Qatar, halikukidhi matakwa yake, lakini likasema litafanya tathmini kabla ya kujibu.