1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaapai kujibu mashambulizi ya Iran dhidi yake

John Juma
16 Aprili 2024

Mkuu wa majeshi ya Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi, ameapa kujibu mashambulizi ya Iran dhidi ya taifa lake, hata baada ya maombi ya viongozi wa dunia wanaohofia migogoro mikubwa ya kikanda kutaka Israel kujizuia.

https://p.dw.com/p/4eqdO
Tel Aviv, Israel | Mkuu wa majeshi ya Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi
Mkuu wa majeshi ya Israel Luteni Jenerali Herzi Halevi akizungumza na maafisa wa jeshiPicha: Israeli Army/AFP

Akiwahutubia wanajeshi katika uwanja wa ndege wa Nevatim ambayo ilipigwa na Iran katika shambulio la Jumamosi usiku, Halevi amesema shambulio la Iran litajibiwa, lakini bila ya kutoa maelezo zaidi.

"Tunatathmini kwa karibu hali ilivyo. Tuko katika tahadhari ya hali ya juu. Vitendo vya Iran vitakabiliwa. Tutachagua jibu letu ipasavyo. Jeshi la Israel bado liko tayari kukabiliana na kitisho chochote kutoka kwa Iran na washirika wake wa ugaidi tunapoendelea na dhamira yetu ya kulinda taifa la Israel.''

Jeshi la Israellimesema idadi kubwa ya silaha hizo zilidunguliwa kwa msaada wa Marekani na washirika wengine, na kwamba shambulio hilo lilisababisha uharibifu mdogo tu.

Soma pia:Israel yaapa kulipiza kisasi dhidi ya Iran

Usiku wa kuamkia leo, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alikutana na baraza lake la vita serikalini kujadili hatua zinazofuata.