1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaapa kujibu mashambulizi dhidi ya ubalozi wa Damascus

2 Aprili 2024

Rais Ebrahim Raisi wa Iran amelaani shambulio la anga la Israel katika Ubalozi mdogo wa Tehran nchini Syria ambalo limesababisha vifo vya majenerali wawili wa Kikosi cha Ulinzi wa Mapinduzi.

https://p.dw.com/p/4eL2J
Iran, Tehran | Ebrahim Raisi
Rais Ebrahim Rais wa Iran ameapa kuwa nchi yake italipiza kisasi mauaji dhidi ya majenerali wake mjini Damascus, Syria.Picha: Rouzbeh Fouladi/ZUMA/picture alliance

Raisi amesema shambulio hilo la Israel mjini Damascus, ambalo miongoni mwa lililowauwa ni majenerali ambao ni Mohammad Reza Zahedi na Mohammad Hadi Haji Rahimi, ni uhalifu wa kigaidi na ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa huku akisisitiza kuwa shambulio hilo litajibiwa.

Soma zaidi: Iran yazidi kuitetea nafasi yake siasa za Mashariki ya kati

"Leo Israel imefanya shambulio sio tu kwa ubalozi wa Iran bali hata katika mji mkuu wa Syria, Damascus. Hatutanyamaza. Tutajibu moja kwa moja kwa sababu wamekuwa wakitushambulia mara nyingi mno. Pia tunaitaka Marekani kusitisha uwepo wake kijeshi nchini Syria." Alisema mmoja wa wakaazi wa mji mkuu huo wa Syria.

Soma zaidi: Kifo cha kiongozi wa Hamas: Unachohitaji kujua kuhusu Hezbollah

Wakati China ikilaani shambulio hilo, kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hizbullah nchini Lebanon linaloungwa mkono na Tehran limeonya kwamba shambulio hilo litajibiwa, na hivyo kuzidisha wasiwasi wa kutanuka kwa mzozo katika eneo zima la Mashariki ya Kati.