1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Georgia yakabiliwa na maandamano zaidi

9 Machi 2023

Georgia inapitia maandamano mapya ya kuipinga serikali huku hasira za umma zikiwa hazionyeshi dalili ya kutulia licha ya chama tawala kuahidi kuachana na sheria ya "mawakala wa kigeni" inayofananishwa na sheria ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4OStr
Georgien | Proteste in Tiflis
Picha: David Mdzinarishvili/AA/picture alliance

 

Chama tawala cha Georgian Dream kilisema mswada wa sheria hiyo ulikuwa umewasilishwa katika namna inayoufanya kuonekana mbya, na kuahidi kufanya mashauriano na umma baada ya kutangaza kuuondoa bungeni. Lakini upinzani haujashawishika na hatua hiyo na umeitisha maandamano mapya leo Alhamisi.

Kishindo cha wapinzani chaubadili mkondo wa serikali Georgia

Kundi la vyama vya upinzani limesema katika taarifa ya pamoja kwamba maandamano hayo hayatasita maadamu hakuna hakikisho kwamba Georgia inachukuwa mwelekeo thabiti wa magharibi. Pia wamedai kuachia mara moja kwa waandamanaji kadhaa waliosema wamezuwilia korokoroni.