1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

China yakanusha tuhuma za ruzuku za magari ya umeme

Mohammed Khelef
8 Aprili 2024

Waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao, amekanusha tuhuma za mataifa ya Magharibi juu ya utowaji wa ruzuku kwa kampuni za magari nchini mwake.

https://p.dw.com/p/4eWWp
Waziri wa Biashara wa China,  Wang Wentao.
Waziri wa Biashara wa China, Wang Wentao.Picha: Florence Lo/REUTERS

Akizungumza siku ya Jumapili (Aprili 7) kwenye majadiliano ya kibiashara mjini Paris, Ufaransa, Wang alisema kampuni za gari za umeme za China hazitegemei ruzuku ya serikali katika kujiiimarisha.

Waziri huyo wa biashara alisema pia kwamba madai ya Marekani na Ulaya juu ya "uwezo uliopitiliza" wa China hayana msigi.

Soma zaidi: China yahadharisha juu ya kuporomoka biashara ulimwenguni

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu (Aprili 8) na wizara yake, Wang yupo mjini Paris kushiriki mazungumzo yaliyotarajiwa kuangazia usafirishaji wa gari za umeme kutoka China kuingia kwenye soko la Ulaya.

Wawakilishi wa zaidi ya kampuni kubwa kumi walitazamiwa kuhudhuria mkutano huo.