1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Burundi yaomba msaada kukabiliana na athari za mvua

18 Aprili 2024

Serikali ya Burundi na Umoja wa Mataifa wametoa wito wa msaada wa kifedha ili kukabiliana na athari mbaya ya mvua mkubwa inayoendelea kunyesha, ambayo imesababisha karibu watu 100,000 kuyahama makaazi yao.

https://p.dw.com/p/4evWG
Evariste Ndayishimiye
Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi.Picha: Tchandrou Nitanga/AFP/Getty Images

Umoja wa Mataifa umeitaja Burundi kuwa miongoni mwa nchi 20 zilizo katika hatari kubwa ya kukabiliwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, wakati mvua isiyo na kikomo tangu mwezi Septemba mwaka jana ikiendelea kuuharibu mji mkuu wa Bujumbura.

Soma zaidi: Burundi yahitaji msaada kukabiliana na mafuriko makubwa

Eneo la Afrika Mashariki limekuwa likikumbwa na mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni ambazo zimegharimu maisha ya takriban watu 58 nchini Tanzania tangu kuanza kwa mwezi huu, huku wengine 13 wakifariki nchini Kenya.