1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Belarus, Urusi zakagua silaha za kimkakati za nyuklia

7 Mei 2024

Belarus imesema imeanza ukaguzi wa kutathmini utayari wa vikosi vyake kuweza kutumia silaha za kimkati za nyuklia.

https://p.dw.com/p/4fayj
Urusi ilipeleka Belarus silaha za nyuklia
Belarus imesema imeanza ukaguzi wa kutathmini utayari wa vikosi vyake kuweza kutumia silaha za nyukliaPicha: Uraltransmash/Tass/IMAGO

Belarus imesema imeanza ukaguzi wa kutathmini utayari wa vikosi vyake kuweza kutumia silaha za kimkati za nyuklia, katika wakati ambapo nchi hiyo ikijiandaa pia na mazoezi ya matumizi yasilaha za nyuklia na mshirika wake Urusi.

Hayo yameelezwa na Shirika la habari la serikali Belta, likinukuu kauli ya Waziri wa Ulinzi wa Belarus Viktor Khrenin aliyesema kuwa Rais Alexander Lukashenko ameamuru ukaguzi wa kushtukiza wa vikosi vinavyosimamia silaha hizo.

Katika hatua ya kukabiliana na mataifa ya Magharibi, Rais Lukashenko alisema mwezi uliopita kuwa "dazeni kadhaa" za silaha za kimkakati za nyuklia kutoka Urusi zilitumwa huko Belarus kufuatia makubaliano yaliyotangazwa mwaka jana kati yake na Rais Vladimir Putin.