1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Haki za Binaadamu kusitisha silaha kwa Israel?

5 Aprili 2024

Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa linajadili iwapo liamuru kusitishwa kwa mauzo ya silaha kwa Israel, ambayo vita vyake huko Gaza vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 33,000, wengi wao wakiwa raia.

https://p.dw.com/p/4eSO7
Volker Turk
Mkuu wa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa, Volker Turk.Picha: Pierre Albouy/KEYSTONE/picture alliance

Iwapo rasimu iliyowasilishwa kwa Baraza hilo siku ya Ijumaa (Aprili 5) itapitishwa, itakuwa ni mara ya kwanza kwa chombo hicho cha Umoja wa Mataifa kuchukuwa msimamo mkali juu ya vita katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa na Israel.

Soma zaidi: Baraza la Usalama lashindwa kupitisha azimio la kusitisha vita Gaza

Rasimu hiyo inatoa wito kwa nchi kusimamisha uuzaji na usambazaji wa silaha na vifaa vingine vya kijeshi kwa Israeli ili kuzuia ukiukaji zaidi wa sheria za kimataifa na ukiukwaji wa haki za binadamu.