1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock amuita balozi wa Urusi

18 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock, amemuita balozi wa Urusi kufuatia kukamatwa watu wawili wenye uraia pacha wa Urusi na Ujerumani kwa tuhuma za ujasusi na kupanga mashambulizi nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4ewMJ
Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani, Annalena Baerbock.Picha: Florian Gaertner/AA/picture alliance

Kulingana na polisi ya Ujerumani, watu hao wawili walikamatwa siku ya Jumatano (Aprili 17) katika jimbo la Bavaria kusini mwa Ujerumani wakidaiwa kuwa katika harakati za ujasusi kwa ajili ya Urusi na kutafuta sehemu za kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Ujerumani.

Soma zaidi: Naibu Kansela wa Ujerumani afanya ziara ya ghafla Ukraine

Baada ya kukamatwa kwa watu hao, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani, Nancy Faeser, alisema Ujerumani isingelitishwa na majaribio ya kijasusi ya Urusi.