1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Austin aghadhibishwa na kuuwawa wafanyakazi wa misaada Gaza

Josephat Charo
4 Aprili 2024

Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin, ameelezea ghadhabu zake kuhusu shambulizi la Israel dhidi ya watoa misaada katika Ukanda wa Gaza katika mazungumzo ya simu na mwenzake wa Israel, Yoav Gallant.

https://p.dw.com/p/4eQ4k
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin.
Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin.Picha: Anna Moneymaker/AFP/Getty Images

Wakati wa mazungumzo hayo ya siku ya Jumatano (Aprili 3), Austin alisisitiza umuhimu wa kuchukuwa hatua madhubti mara moja kuwalinda wafanyakazi wa kutoa misaada na raia wa Palestina huko Gaza, baada ya juhudi za pamoja na mashirika ya misaada ya kigeni kushindwa mara kadhaa.

Soma zaidi: Biden kuzungumza na Waziri Mkuu wa Israel Netanyahu

Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Marekani, Pat Ryder, alisema Jumatano jioni kwamba Waziri Austin alimhimiza Gallant afanye uchunguzi wa haraka na wa wazi kuhusu tukio hilo la mauaji ambapo wafanyakazi saba wa shirika la misaada la World Central Kitchen waliuwawa siku ya Jumatatu (Aprili 1).

Austin alitaka matokeo ya uchunguzi huo yatangazwe hadharani na waliohuska wawajibishwe.